Kozi hii inalenga wanafunzi ambao Kiswahili ni lugha geni kwao .  Kwa sabubu hii,  inalenga kufundisha stadi zote za mawasiliano ili kumwezesha mwanafunzi kuwasiliana kwa kiwango cha chini katika kiswahili. 

Madhumuni ya kozi hii ni kuwahimiza wanafunzi kutumia lugha sanifu katika mawasiliano na pia maandishi. Wanafunzi wanatarajiwa kubainisha maana ya misamiati mbalimbali huku wakizingatia ufasaha wa lugha kisarufi. Aidha, mwanafunzi anatarajiwa kuimarisha stadi mbalimbali kuhusiana na kusoma,kusikiliza, kuandika na kusema.