Kozi hii inachunguza dhana ya lugha na kazi yake katika jamii. Lengo kuu la kozi hii ni kuchunguza dhana ya lugha kimuundo na kimatumizi. Vipengele vya kimsingi vitakavyoshughuliwa ni pamoja na: dhana ya lugha, dhana ya lahaja: historia ya Kiswahili, maendeleo, ukuaji na matumizi yake: sarufi, uakifishaji, na insha mbalimbali. Kupitia somo hili, utapata ilhamu, motisha na changamoto ya kukitumia Kiswahili sanifu katika maandishi na vilevile katika maingiliano ya mazungumzo ya kila siku katika jamii. Hivyo basi, unatarajiwa kupiga vita makosa ya kimaendelezo na pia ya kisarufi ama katika mazungumzo au maandishi ya katika kutumia lugha ya Kiswahili katikamaandishi au katika mazungumzo katika shughuli na mitagusano mbalimbali.