Katika somo hili tunaangazia upangaji wa lugha pamoja na  uundaji na uendelezaji wa sera za lugha.

Katika  somo hili tutaangazia lugha ya Kiswahili na jinsi inavyoendelezwa katika sekta mbalimbali za serikali na chini ya uangalizi wa mashirika yasiyo ya serikali.

Wanafunzi wanatakiwa kujifahamisha na kauli rasmi katika katiba ya Kenya pamoja na wizara mbalimbali zinazotumia lugha ya Kiswahili katika nyanja tofauti. Makala nyingi zitapatikana kwenye mtandao na maktabani.