Kozi hii inachunguza uundaji wa maneno, mpangilio, kanuni na mahusiano ya maneno katika sentensi ya lugha. Vipengele muhimu vitakavyochunguzwa vitatokana na mofolojia na sintaksia. Isitoshe, kozi hii inatoa maelezo ya kimsingi kuhusu dhana ya mofolojia na sintaksia ya Kiswahili.  Kozi hii basi, inaazamia kufafanua dhana za kimsingi za mofolojia na sintaksia kama vile: mofu, mofimu, alomofu, maneno, uambishaji, uundaji maneno, uainishaji wa ngeli kimofolojia na kisintaksia, vipengele amilifu vya kisintaksia kama vile: virai, vishazi, sentensi, kategoria za maneno, kategoria amilifu, aina za virai, aina za sentensi, uambajengo, uundaji wa miundo mbalimbali, ukilishaji wa sentensi katika matawi, mishale, jendwali na matawi.  Vile vile kozi hii itachunguza maingiliano ya mofolojia na sintaksia:  maingiliano na kuachana kwa dhana hizi mbili na vile vile itashughulikia nadharia za kisintaksia.

Mofolojia na sintaksia hufaana na kukamilishana katika ulewa wa maneno na sentensi ya lugha.

Kozi hii basi itakupa ilhamu ya kuzamia katika taaluma ya uelewa  wa mofolojia na sintaksia ili uweze kubwia kanuni na kuwa na umilisi mzuri wa lugha yako na kuweza kuitumia lugha ipasavyo kimatamshi na kimaandishi.