Kozi hii inatoa maelezo ya kimsingi kuhusu dhana ya mofolojia na sintaksia ya Kiswahili.  Kozi hii basi, inazamia kufafanua dhana za kimsingi za mofolojia na sintaksia kama vile: mofu, mofimu, alomofu, maneno, uambishaji, uundaji maneno, virai, vishazi, sentensi, kategoria za maneno, kategoria amilifu, aina za virai, aina za sentensi, uambajengo, uundaji wa miundo mbalimbali na maingiliano ya mofolojia na sintaksia na vile vile nadharia za kisintaksia.