Kozi hii inatalii kwa undani namna ya kutamka sauti mbalimbali za lugha kwa kutumia viungo au ala za utamkaji.  Zaidi,’ inafafanua namna sauti za lugha zinavyotamkwa, kusikika masikioni mwa binadamu na namna sauti hizo zinasafirishwa hadi ubongoni mwa binadamu ili kufanyiwa fasiri mbalimbali.  Kwa sababu hii, mwanafunzi anapaswa kuelewa mchakato mzima wa matamshi na kutambua umuhimu wa matamshi bora katika matumizi ya lugha ya kila siku. Kwa mantiki hii, anastahili kuhusisha matamshi na maana na vile vile, aelewe uhusiano wa ubongo wa mwanadamu na matamshi.