Kozi hii inachunguza dhana ya maana katika lugha.  Maana zitakazochunguzwa ni maana msingi na ya kimuktadha.  Maana kimsingi inahusishwa na semantiki, na kwa upande mwingine maana kimuktdha unahusishwa na semantiki.  Dhana hizi mbili hufaana na kukamilishana katika uelewa wa maana katika mawasiliano ya lugha.  Utengano katika ya semantika na uamali huwa ni finyu sana kwa kuwa kila inalenga maana. Kozi hii basi itakupa ilhamu ya kuzamia katika taaluma ya uelewa wa maana.