Kozi hii inachunguza uundaji wa maneno,  mpangilio, kanuni na mahusiano ya maneno katika sentensi ya lugha. Vipengele muhimu vitakavyochunguzwa vitatokana na mofolojia na sintaksia. Kozi hii basi, inatoa maelezo ya kimsingi kuhusu dhana ya mofolojia na sintaksia ya Kiswahili.  Kwa hiyo, kozi hii  inazamia kufafanua dhana za kimsingi za mofolojia na sintaksia kama vile: mofu, mofimu, alomofu, maneno, uambishaji, uundaji maneno, uainishaji wa ngeli kimofolojia na kisintaksia.