Kozi hii inalenga kukufundisha kuhusu mambo ya kimsingi katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Madhumuni ya kozi hii  basi ni kukuhimiza kama mwanafunzi kutumia lugha sanifu katika mawasiliano ya midomo na maandishi. Hivyo, unatarajiwa kubainisha aina ya maneno, maana ya sarufi,  maana ya misamiati mbalimbali na matumizi yake na kadhalika.  Kozi hi kwa jumla itakuimarisha na stadi mbalimbali kuhusiana na kusoma, kusikiliza, kuandika na kadhalika.