Kozi hii inachunguza dhana ya maana katika lugha. Maana zitakazochunguzwa ni maana msingi na maana kimuktadha. Maana kimsingi inahusishwa na semantiki, na kwa upande mwingine maana kimuktdha uhusishwa na pragmatiki. Dhana hizi mbili hufaana na kukamilishana katika uelewa wa maana katika mawasiliano ya lugha. Utengano kati ya semantika na uamali huwa ni finyu sana kwa kuwa kila inalenga maana ila kwa mitazamo tofauti. Kozi hii basi itakupa ilhamu ya kuzamia katika taaluma ya uelewa wa maana.