Kozi hii inachunguza lugha kiisimu. Isimu ni dhana inayochunguza lugha kisayansi. Kozi hii basi, ni msingi wa kozi zote za tanzu za isimu. Vipengele vya kimsingi vitakavyoshughukikiwa katika kozi hii ni pamoja na dhana ya lugha, usuli wa lugha, sifa za lugha, dhana ya isimu, malengo ya isimu, matawi ya isimu, tofauti ya lugha ya binadamu na ya wanyama, tipolojia ya lugha, leksikolojia na leksikografia miongoni mwa mada nyingine. Lengo la kozi hii ni kuchunguza lugha kisayansi na kuweza kuwekea misingi dhana muhimu zinazohusiana na isimu ya lugha. Kwa hiyo, kozi hii itakupa ilhamu ya kuzamia katika taaluma ya isimu na kuweza fafanua lugha kidhana ya kimuundo.