Kozi hii inachunguza dhana ya lugha na kazi yake katika jamii.  Lengo kuu la kozi hii ni kuchunguza dhana ya lugha kimuundo na kimatumizi.  Vipengele vya kimsingi  vitakavyoshughuliwa ni pamoja na: dhana ya lugha, dhana ya lahaja: historia ya Kiswahili, maendeleo, ukuaji na matumizi: sarufi, uakifishaji, na insha mbalimbali.   Kupitia somo hili, utapata ilhamu, motisha na changamoto ya kukitumia Kiswahili sanifu katika maandishi na vilevile katika maingiliano ya kimazungumzo ya kila siku katika jamii. Hivyo basi, unatarajiwa kupiga vita makosa ya kimaendelezo na pia ya kisarufi ama katika kutumia lugha ya Kiswahili  katikamaandishi au katika mazungumzo katika shughuli na mitagusano mbalimbali.