Mhutasari wa Kozi:

Kozi hii inachunguza na kuchanganua dhana ya  isimu maana ambayo katika viwangi vya ufundishaji wa lugha, ndiyo hurejelewa kama Semantiki. Maana ya kimsingi,uhusishi na ya kimuktadha katika maandishi na mazungumzo mbalimbali. Mwanafunzi atatanabahishwa umuhimu wa matumizi ya lugha kwa jumla kwa kuzingatia maana. Aidha, atatanabahishwa jinsi matamshi na muktadha huathiri maana ya lugha kiisimu. Hali kadhalika, kozi hii itatoa utangulizi wa mipaka ya sematikai na uamali (Pragmatiki), dhima ya uamali katika mazungumzo, maandishi, fasii na ubainishaji wa kauli na ukweli.